Resultaat vir "Category: Happiness and peace"


Warning: count(): Parameter must be an array or an object that implements Countable in /home1/promised/public_html/wp-content/plugins/assensive-widgets/widgets/ASSENSIVE_WIDGET_POST_GRID.php on line 913
Mwezi wa Rajab, ni mwezi wa kumiminika kwa rehema a Allah
Mwezi wa Rajab, ni mwezi wa kumiminika kwa rehema a Allah Je, inawezekana vipi mtu akawa ndani ya adhabu ya moto wa Jahanamu, lakini ghafla adhabu ikakatika na kisha mtu yule kutolewa na kupelekwa peponi?
Mwezi wa Rajab, ni fursa kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa moyo.
Mwezi wa Rajab, ni fursa kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa moyo. Mwezi wa Rajab, ni mwezi wa kumiminika kwa rehema za Mwenyezi Mungu (swt), sasa je, sisi tupo katika hali ya kuweza kupokea hizo rehema zake kwa kiwango cha juu?
Je, thamani ya mwanadamu inapatikana wapi?
Je, thamani ya mwanadamu inapatikana wapi? Je, mwanadamu huwa anafanya mambo gani kiasi kwamba baada ya muda mfupi moyo huu hufa? Je, uhakika wa mwanadamu unapatikana wapi?
Ni wapi au ni kutoka kwa nani unaweza kupata maelezo kamili juu ya furaha?
Ni wapi au ni kutoka kwa nani unaweza kupata maelezo kamili juu ya furaha? Je, ni kutoka kwa mtu mwenye elimu kwa ngazi ya juu? Au ni kutoka kwa mtaalamu wa maswala ya saikolojia? Mimi kwa mtazamo wangu ni kwamba, yupo moja tu ndiye mwenye uwezo wa kutoa maelezo kamili na sahihi juu furaha, naye ni Mwenyezi Mungu tu. Kwa mtazamo wako, Mwenyezi Mungu anaielezea vipi furaha?
Nyakati bora kabisa
Nyakati bora kabisa Hebu jaribu kuvuta picha kwamba upo ndani ya vazi la kifalme lenye kunakshiwa na dhahabu nzuri kabisa, huku kichwani mwako ukiwa umeweka kofia ya kifalme yenye kunakshiwa pia na yakuti nyekundu, na kwa upande mwingine kuna malaika wazuri ambao wapo pembeni ya mango wa pepo wakikwambia: “..Kwa furaha na heshima, ingia peponi..” Aaaah!, ni wakati mzuri ulioje. Kuingia sehemu ambayo ni ya kudumu na milele! Kwa mtazamo wako, unadhani kuna sehemu au nyakati bora zaidi ya hii?
Ni upi uhakika na ukweli wa furaha ya watu wa peponi?
Ni upi uhakika na ukweli wa furaha ya watu wa peponi? Furaha ndani ya pepo itakuwa ni katika msingi wa kwamba siku hadi siku itakuwa ni yenye kutuweka karibu na Mwenyezi Mungu. Sasa kiuhalisia watu wa peponi duniani pia walikuwa hivi hivi, kwa maana ya kwamba pia walikuwa ni watu ambao walichagua furaha ambayo siku hadi siku ilikuwa ni yenye kuwasogeza kwa Mwenyezi Mungu. Kiukweli ni kwamba hakuna kabisa furaha ya juu zaidi ya ile yenye kukusogea karibu na Mwenyezi Mungu. Kwa mtazamo wako, ni furaha zipi ambazo zina sifa ya kutusogeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Tafadhali hebu tuandikie katika comment
Mazazi salama ya mtoto huwa ni furaha na fanaka kwa wazazi wa mtoto yule.
Mazazi salama ya mtoto huwa ni furaha na fanaka kwa wazazi wa mtoto yule. Hivyo nasi pia, tunaweza kuwa ni sababu ya kufurahi kwa wazazi wetu wa mbinguni na kiroho kutokana na aina sahihi ya maisha yetu. Kama ambavyo tuna uwezo wa kuandaa hii furaha ya hawa wazazi wetu na kuifanya kuwa ni furaha ya kudumu milele. Sasa ni vipi tunaweza kuwa na uzawa salama huo ahera?
Tusiwe ni wenye kuchukulia ugumu sana katika maisha yetu!
Tusiwe ni wenye kuchukulia ugumu sana katika maisha yetu! Kumbuka ya kwamba kila ambapo tunakumbana na matatizo, basi tunakuwa ni mfano wa mto ambao kadri ambavyo unakutana na mawe makubwa ndivyo ambavyo unazidi kuwa ni wenye maji matamu zaidi. Hebu na sisi tuwe ni mfano wa mto na mawe makubwa, tupite haya matatizo yetu na tuache yenyewe ndio yabakie na zile aibu na uchafu wa roho zetu. N vipi tunnaweza kufikia hatua ya kuwa na roho safi ? Tafadhali hebu tuandikia maoni yako katika Comment.
Kilele cha kushuhudia mazuri na mema
Kilele cha kushuhudia mazuri na mema Moja kati ya neema kubwa mno ni pamja na neema ya macho, macho ambayo kuitia yenyewe tunaweza kushuhudia na kuna uzuri wa uumbaji. Sasa kuna mambo mengi mno ambayo hayana kabisa thamani ya kuyatazama, kwa mfano kutazama na kushuhudia aibu za wengine. Sasa haya ndio yale mambo ambayo kutoyatazama huwa kunatujaza hali ya utulivu, kama ambavyo pia huwa yanamfurahisha Mwenyezi Mungu. Je, unadhani ni sahihi kumkasirisha Mwenyezi Mungu mwenye huruma, muumba wa kila kitu, kwa sababu tu ya kitu kidogo? (kutazama yasiofaa)
Msingi wenye nuru
Msingi wenye nuru Dunia ni sehemu na uwanja wa mitihani, lakini pepo ni sehemu ya kudumu milele. Na jambo pekee ambalo Mwenyezi Mungu analihitaji katika maisha yetu ya dunia, ni juhudi na jitihada zetu tu, kwa mfano tufanye juhudi kwa ajili ya kuwa watu bora. Lakini cha ajabu ni kwamba wengi wetu huwa tunasubiria matokeo yake hapa hapa duniani!. Je, unadhani maisha ya ahera na yenye kudumu hayana thamani ya sisi kujitoa na kuvumilia machungu na magumu ya dunia?
Kuna huzuni ambazo huwa ni sababu ya furaha zetu
Kuna huzuni ambazo huwa ni sababu ya furaha zetu Kuna baadhi ya huzuni ni kweli hazina faida kabisa, kwa maana si kwamba ni zenye kuharibu na kutibua usalama wa miili yetu tu, bali pia huharibu nakutibua usalama wa roho zetu. Lakini una baadhi ya huzuni nyinginezo, zenyewe kwa dhahiri ni huzuni, lakini ndizo zenye kutupa furaha na kutujaza nguvu. Sasa hauoni kwamba ni vyema tukawa ni wenye kuzifuatilia? Unadhani inawezekana kweli huzuni ikawa ni yenye kusababisha furaha? Hebu tafadhali tuandikie mawazo yao katika comment!
Hebu tuishi na huu msingi!
Hebu tuishi na huu msingi! Inawezekana ikawa ngumu kwetu kutambua kuwa mazoezi yana uwezo kiasi gani katika maisha yetu, ikiwa na pamoja na athari zake zenye kuleta uchangamfu kwetu. Uchangamfu ambao utapatikana katika miili yetu, na mwingine katika roho zetu. Lakini pamoja na hayo bado tumekuwa tukiishi katika hali ya uzembe na kuyakimbia hayo mazoezi, tena kila leo na kesho. Angalia, usalama na afya ni katika neema kubwa mno, ambazo endapo tutazipoteza basi haitakuwa salama kwetu kabisa.
Kwa hakika bila ya Mwenyezi Mungu basi maisha yanapita wa tabu mno!
Kwa hakika bila ya Mwenyezi Mungu basi maisha yanapita wa tabu mno! Na kwa minajili hiyo, ndio maana jambo la msingi zaidi katika maisha yetu, ni kuhakikisha kuna uhusiano wa kweli, wenye nguvu na kudumu baina yetu na Mwenyezi Mungu. Mwenyezi mungu ambaye daima yupo pamoja na sisi, au kama ambavyo mwenyewe ametuambia kwamba yupo karibu nasi zaidi ya mshipa wa koo. Kwa hakika kwa kitendo cha sisi kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, ndipo ambapo kunapatikana furaha ya kweli, furaha ambayo haitakuwa ni yenye kutetereka kwa sababu tu ya kutokuwa na vitu vingi. Hivi unadhani ni kwa nia zipi tunaweza kuanzisha uhusiano mzito na wa kweli na Mwenyezi Mungu swt?
Kamwe, usijaribu kufananisha dhahiri ya maisha ya wengine na undani wa maisha yako!
Kamwe, usijaribu kufananisha dhahiri ya maisha ya wengine na undani wa maisha yako! Je, umeshawahi kukutana na mtu ambaye ana maisha ya chini na ya kawaida, lakini moyo wake ni wenye utulivu na furaha siku zote? Au umeshawahi kukutana na mtu ambaye ana utajiri na mali nyingi pamoja na uwezo, lakini siku zote ni mwenye mawazo, msongo wa mawazo na huzuni? Sasa hii maana yake ni kwamba utulivu haupatikani kupitia mali wala utajiri, Bali utulivu unapatikana katika kujenga uhusiano wenye nguvu na upendo na Mwenyezi Mungu swt. Je, tuo tayari tuanzishe huu uhusiano wa upendo na Mwenyezi Mungu?
Wala sio hiyo njia ya utatuzi wake!,
Wala sio hiyo njia ya utatuzi wake!, Kwa maana kila jambo lina njia yake ya utatuzi, muhimu tu ni kujua na kuipatia njia ile. Kujiua sio njia tatuzi ya kuepukana na magumu! Na ikitokea tukajisalimisha au tukashindwa kupambana na magumu basi ni kutokana na udhaifu wetu. Kwa maana magumu yote ambayo hutokea katika maisha yetu basi ni kwa ajili ya kutujenga na kutukuza Sasa je, unaona ni sahihi kupambana na kukabiliana na magumu kwa ajili tu ya kufikia katika ufaulu na ukubwa?
Bila shaka kuna mambo mazuri mengi mno ambayo hutokea katika maisha yetu
Bila shaka kuna mambo mazuri mengi mno ambayo hutokea katika maisha yetu Kama ambavyo mambo mengi mno ambayo hutokea katika maisha yetu, huwa ni sababu ya mabadiliko fulani katika maisha yetu haya. Mfano mzuri ni ile mipangilio mizuri ambayo huwa ndio sababu ya kuwa na natija nzuri, na bila shaka mambo haya huwa ni sababu ya kufurahi kwetu!. Saa je, tupo tayari kutenga muda wetu kwa ajili ya mabadiliko makubwa na mazuri?